Bastola ya majambazi wa Kolonia Santita iitwayo Akdal Ghost kutoka Uturuki, yenye uwezo wa kubeba kwa wakati mmoja risasi kumi na tano katika chemba yake, iliyokamatwa na Polisi wa Tume ya Dunia huko Varsovia nchini Meksiko.
http:www.enockmaregesi.wordpress.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...

-
Mercury Cougar ya John Murphy aliyonunua mwaka 1990 kwa gharama kubwa huko Michigan nchini Marekani. Gari hilo lililorekebishwa kwa ajili ...
-
120. Wakati mwingine tukitaka kutambulika hatuna budi kuweka mbele aibu ya heshima yetu. http://www.enockmaregesi.wordpress.com
-
179. Yesu alipokuwa msalabani watu wengi walimzunguka. Askari wa Kirumi aliyekuwa na chongo, na mkuki, alikuwa na jukumu la kumtesa Yesu ...
Akdal Ghost ni bastola iliyokuwa imetengwa kuwaua Vijana wa Tume John Murphy na Frederik Mogens lakini wakasaidiwa na Mtoto wa Rais Debbie Patrocinio Abrego na walinzi wake. Hata hivyo majambazi waliokuwa wametumwa kufanya kazi hiyo walikamatwa kabla hawajatekeleza jukumu lao, na kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Tume ya Dunia cha Zona Rosa kwa ajili ya mashtaka. Lakini hawakushtakiwa. Walipewa msamaha, wa Programu ya Ushahidi ya Tume ya Dunia ('WODEA Protection Programme') kwa makubaliano ya ushirikiano wa asilimia 100 katika kesi dhidi ya makamanda wa Kolonia Santita.
ReplyDeleteWWPP ('WODEA Witness Protection Programme') ni Programu Maalumu ya Ushahidi ya Tume ya Dunia ya kuwakinga mashahidi wa kihalifu kwa kuwapa makazi mapya, majina mapya, kazi mpya, historia mpya ya maisha, na sura mpya, kuwakinga na Sheria ya Kitalifa ya Kolonia Santita. Ukivunja Sheria ya Kitalifa ya Kiapo cha Swastika cha Kolonia Santita utauwawa, tena utauwawa kinyama, wewe na familia yako.
ReplyDeleteKitalifa ni utiifu kamili, woga, umbali (kwa maana ya kuwa mbali na biashara ya mamafia wengine mpaka kwa makubaliano maalumu) na nidhamu ya kutoshirikiana na mamlaka zote za serikali. Ukishtakiwa kwa kosa la madawa au ujambazi ambalo hukufanya, utatumikia kifungo mpaka mwisho bila kushirikiana na polisi (kwa maana ya kutaja aliyehusika au waliohusika na uhalifu huo) hata kama aliyehusika au waliohusika hana au hawana uhusiano wowote na Kolonia Santita. Falsafa ya Kitalifa ni Sheria ya Kitalifa ya Kiapo cha Swastika cha Kolonia Santita. Na adhabu ya kuvunja sheria hiyo ni kifo.
ReplyDelete