Adam Kuambiana umerudi nyumbani ulikotoka, ukiongozwa na imani na mwanga wa 
wale uliowapenda na kuwapoteza. Hatuwezi kukumbuka kwamba umetutoka bila 
kukumbuka kwamba uliishi, na kwamba maisha yako yalitupa kumbukumbu nzuri 
tusizoweza kuzisahau haraka. Jumanne, siku ya kuuaga mwili uliokuwa ukitumiwa na 
wewe, wengine watasema Kwa heri lakini mimi nitasema Asante! Asante kwa sababu 
ya kipaji chako. Asante kwa sababu ya kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wako wote, 
kutoa sauti kwa wale wote waliokuwa hawawezi kusikika. Asante kwa sababu ya 
kuacha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta wakati ukiingia, na Asante kwa 
sababu ya maisha yako. Tukiendelea kuomboleza kifo cha Adam Kuambiana hapa 
duniani, wengine wanasherehekea kukutana naye huko mbinguni. Mchungaji wa uhai 
wa wote Mungu wa mbinguni ailaze roho yake mahali pema peponi: Yeye ni mwandishi 
wa hadithi ya maisha yetu na ndiye aliyeandika ukurasa wa mwisho wa hadithi ya 
Adam.
http://www.facebook.com/koloniasantita 
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
- 
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
 - 
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
 
Maisha ya watu yamebadilika kwa sababu Adam Kuambiana alikuwepo hapa.
ReplyDeleteMay God Bless Adam Kuambiana, and may he rest in eternal peace.
ReplyDeleteRest in Peace, Man!
ReplyDelete