Friday, 4 October 2013

Sittard

Sittard,
Ndege ya Murphy (Air France Flight 279 Boeing 747-400) ilipoanguka ikiwa njiani kuelekea Copenhagen nchini Denmaki; kutokea Tanzania, Uholanzi na Ufaransa.

http://www.enockmaregesi.com

2 comments:

  1. Ndege ya Shirika la Ndege la Ufaransa, Air France Flight 279 Boeing 747-400, ndege ya Murphy, mara tu baada ya kukaa sawa angani futi 31,000 juu ya usawa wa bahari; mara tu baada ya rubani kuwasiliana na wenzake waongoza ndege akiwajulisha kuwa sasa alishakaa vizuri angani, ililipuka kwa kishindo kikubwa na kuanza kushuka kwa mwendo mkali kama risasi ya marisau. Chini, katika mji wa Sittard, watu walikuwa wakiendelea na shughuli zao kama kawaida; vipande vya ndege vilipojibamiza kwenye ardhi na kuacha shimo (kubwa) lenye ujazo wa tani 1500 za udongo na mawe. Vipande vya ndege vilisambaa (vikiwa hewani) katika eneo kubwa kama jiji la Dar es Salaam, zaidi ya kilomita za mraba 1500, na kukata mawasiliano yote ya simu na faksi katika eneo lote la kusini mwa Uholanzi. Zaidi ya polisi 1000 na wanajeshi 600, walizagaa katika eneo la ajali (‘epicenter’) na bila kuchelewa wataalamu wakahitimisha kwamba; Air France 279 ililipuka ikiwa angani, kabla hata haijafika chini. Watu 7 kutoka Sittard walikufa, pamoja na watu 304 (wote) waliokuwemo ndani ya ndege ya Shirika la Ndege la Ufaransa.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...