Monday, 30 September 2013

Watu

52. Watu wakikuonyesha tabia zao za ndani kabisa waamini. Wanajijua vizuri zaidi, kuliko unavyowajua.

http://www.facebook.com/koloniasantita

4 comments:

  1. Falsafa ya Watu ilihamasishwa na Dr Maya Angelou wa Marekani.

    ReplyDelete
  2. Watu wakikuonyesha tabia zao za ndani kabisa usisubiri wakuonyeshe tena ndiyo uwaamini. Waamini kwa mara ya kwanza. Mtu, kwa mfano, akionyesha kwa mara ya kwanza kuwa si mwaminifu mwamini. Anajijua zaidi kuliko unavyomjua. Aidha, mtu akikwambia anakupenda halafu akakupiga ni mnafiki. Maneno yake yatasema anakupenda, vitendo vyake vitasema hakupendi. Ukiwa makini na matendo ya mtu, si maneno yake, utamjua. Sikiliza maoni ya watu! Kuwa makini na matendo ya mtu.

    ReplyDelete
  3. Rafiki mzuri ni yule mnaesaidiana ktk shida na raha,ikitokea rafiki yako akakukimbia wakati wa shida bac ujue si rafiki mzuri huyo na hiyo ndiyo tabia yake unapaswa kuiamini.

    ReplyDelete
  4. Wengi ni wanafiki hivyo kujua tabia za watu muhimu

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...