KOLONIA SANTITA TANZANIA
Jalada jipya la kitabu cha Kolonia Santita: Laana Ya Panthera Tigrisi, kitakachochapishwa tena nchini Tanzania hivi karibuni. Wapenzi wote wa riwaya za kijasusi wa Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Ethiopia, Jibuti na Kongo, maji yamekuja ya kumaliza kiu yenu. Tofauti na Kolonia Santita Amerika (sentimita 14.9 kwa sentimita 22.6), Kolonia Santita Tanzania kitakuwa kidogo (sentimita 12.9 kwa sentimita 19.9) na kitagawanywa mara mbili – sehemu ya kwanza na ya pili – na yale yote ambayo hayakuwemo kwenye Kolonia Santita Amerika, yatakuwemo kwenye Kolonia Santita Tanzania! Muda wa kucheza umekwisha.
http://www.enockmaregesi.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
- 
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
 - 
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
 

Sehemu ya kwanza ya Kolonia Santita Tanzania itaisha kwa utamu wa hali ya juu ('cliffhanger') kuhusu Rais wa Tume ya Dunia – kitu ambacho hakikuwemo kwenye Kolonia Santita Amerika – na sehemu ya pili itaisha kwa utamu wa hali ya juu kuhusu lengo ('motive') hasa la Kolonia Santita, ambalo kadhalika halimo kwenye Kolonia Santita Amerika.
ReplyDeleteWakati huohuo kaeni tayari kwa kitabu kipya kitakachochapishwa nchini Marekani mwaka ujao (jina limefichwa) kitakachohusu mapenzi na mauaji ya kimafia. Hiki (kitabu kizuri sana, pengine kuliko 'Kolonia Santita') kimechezewa ('set') Dar es Salaam, Nairobi, Paris, na Los Angeles, California. Wahusika wakuu ni Katherine (ubini umefichwa), Kennedy (ubini umefichwa), na Patrick (ubini umefichwa). Katherine ni mwanamitindo maarufu duniani na mzuri wa kupindukia kutoka Nairobi nchini Kenya. Kennedy amemaliza kidato cha sita, bahati inamwangukia anapokutana na Katherine katika mazingira ya kutatanisha. Kennedy, ambaye bado hajapata kazi na mbangaizaji wa mjini, anakaa Victoria mjini Dar – jirani na Neema (ubini umefichwa), mpenzi wake wa siku nyingi. Patrick ni mfanyabiashara tajiri wa kupindukia kutoka Nairobi nchini Kenya, mwenye makadirio ya utajiri wa dola za Kimarekani milioni 750.
Patrick na mke wake (Katherine – mke wake wa pili) wana nyumba kubwa ya kifahari mjini Dar (karibu na Victoria), Paris (ambako Katherine ana kiwanda cha nguo na ofisi ya kimataifa ya uwakala wa mitindo), Sydney na Los Angeles ambako Katherine alisomea mitindo na biashara kwa mpangilio huo. Mapenzi yanamwingiza Kennedy katika matatizo makubwa – kuliko yeye na familia yake walivyoweza kufikiria – kutoka Kenya, Tanzania na Marekani. Watu zaidi ya ishirini wanapanga kumuua kennedy kinyama, lakini Katherine (na marafiki zake na wazazi wake, na baadhi ya walinzi wa Patrick) atamlinda kwa gharama yoyote – hata kifo!
Nakisubiri hicho kitabu kipya kwa hamu sana, Enock!!!
DeleteNakutakia kila la kheri katika shughuli zako zote za uandishi Enock Maregesi.
ReplyDeleteAsante sana, David Mwakayumba.
DeleteNi maoni yangu kwamba Kolonia Santita Tanzania kitakuwa kizuri kuliko Kolonia Santita Amerika, kwaa sababu ya information mpya itakayoingizwa KST. Niwekee copy yangu please!!!!!
ReplyDelete