Thursday, 12 September 2013

Madawa

Madawa ya kulevya yaliyotumika katika kitabu cha Kolonia Santita: Laana Ya Panthera Tigrisi. Kokeini, tani 183. Heroini, tani 90. Methamfetamini, tani  81. Eksitasi, tani 27.54. Bangi, tani 186. Uyoga wa kichawi, tani 60.

4 comments:

  1. Kolonia Santita ilikuwa na tani 627.54 za madawa ya kulevya ilizokuwa imezikusanya kwa siri kwa muda wa miezi 9 mfululizo. Ilikuwa imepanga kuzisafirisha ndani ya siku 10 baada ya kutokea kwa mauaji ya Tijuana-San Diego, katika mpaka wa Meksiko na Marekani; kwenda Asia, Afrika, Amerika, Ulaya na Australia, kabla ya kukamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya na Ugaidi wa Kimataifa Duniani WODEA. Kokeini tani 183, heroini tani 90, methamfetamini tani 81, eksitasi tani 27.54 (vidonge milioni 110.16). Bangi tani 186, uyoga wa kichawi tani 60. Madawa hayo yalikuwa na thamani ya mtaani ya shilingi za Kitanzania trilioni 12.9.

    Lengo kuu la Kolonia Santita kuuza madawa hayo ni kuwafadhili askari wa msituni wa Kolombia (magorila wa vyama visivyokuwa rasmi vya kisiasa au vyama haramu vya kisiasa) kushika hatamu za uongozi wa Kolombia, kwa makubaliano ya Kolonia Santita kutawala biashara ya kokeini ya taifa hilo la Amerika ya Kusini. WODEA lazima ilizuie Shirika la Madawa ya Kulevya la Kolonia Santita kuuza madawa hayo kwa gharama yoyote ile, pesa au damu, kutetea afya na amani ya dunia.

    ReplyDelete
  2. Madawa ya kulevya hayawezikuwa eradicated kwa sababu hata serikali inayatumia kwa ajili ya afya na utabibu (vitu ambavyo ni vya muhimu kwa maisha ya watu).

    ReplyDelete
  3. your book is very convincing that's how novels are supposed to be.

    ReplyDelete
  4. kokeini ilimuua rafiki yangu kipezi Anastazia sitakaa niisahau milele

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...