Monday, 16 September 2013

Kujitolea

50. Nilijitolea sehemu ya maisha yangu ya kijamii na kifamilia kuweza kuchapisha Kolonia Santita katika kiwango nilichokitaka.

http//www.facebook.com/koloniasantita

3 comments:

  1. Kuvunja laana za mababu zetu (‘generational curses’, laana ambazo hatukushiriki lakini leo zinatusumbua), tunatakiwa wakati mwingine kujitoa mhanga. Kufanikiwa katika maisha ni kuwa tayari muda wowote kujitoa mhanga kwa ajili ya kitu unachoweza kuwa. Miaka kumi na nane iliyopita, mwaka 1995 kwa uhakika zaidi, nilijiwekea nadhiri juu ya maisha yangu: Kufufua mwamko wa usomaji wa vitabu kwa ajili ya kizazi hiki na vizazi vijavyo, kuwa mtetezi wa lugha ya Kiswahili katika kipindi chote nitakacho kuwa hai, na kuwa mwandishi bora wa vitabu Tanzania. Nilijitolea vingi katika maisha yangu kuandika na kuchapisha KOLONIA SANTITA katika kiwango cha kimataifa, na KOLONIA SANTITA ni kitu pekee katika maisha yangu kilichofanya niridhike. Ukifanya maamuzi kubaliana na matatizo yake.

    ReplyDelete
  2. Huwezi kujitolea ('sacrifice') bila kukubaliana na matatizo ya maamuzi yako.

    ReplyDelete
  3. Uvumilivu ni muhimu sana katika kufanikiwa katika maisha.hakika umeonyesha uvumilivu wa hali ya juu sana!

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...