Monday 26 February 2018

Kula, Lazima Tuue!

266. Maisha ni muuaji na yanatulazimisha kuishi. Kula, lazima tuue!

Kama maisha ni muuaji na yanatulazimisha kuishi, uhuru wa kuchagua tutautoa wapi? Mathalani, bila chakula au hewa tutaishi vipi? Tuna uhuru wa kuchagua mema au mabaya, lakini hatuna uhuru wa kuchagua mambo mengine. Hatuna jinsi. Lazima tule. Lazima tuvute hewa.

Kila tunapokula na kunawiri kama binadamu tunakula kitu ambacho hapo awali kilikuwa kikiishi, lakini sasa kimekufa. Kondoo analiwa akiwa hai, au akiwa amekufa, lakini hicho kipande kinacholiwa akiwa hai au amekufa seli zake zimekufa. Tunalazimishwa kula vitu ambavyo tayari vimeshakufa.

Kwa mfano, kuna watu hawapendi kula. Wanalazimisha tu. Lakini hawana jinsi. Lazima wale ili waishi. Hata hivyo, hali hiyo hubadilika unapoingia Asiyah. Asiyah ni sayari ya kwanza ya ulimwengu wa roho. Sayari nyingine za ulimwengu wa roho ni Yetzirah, Beriah, Atzilut na Adam Kadmon. Adam Kadmon ndipo anaposemekana kuishi Mungu.

Sayari zote hizo zimetajwa kimafumbo katika kitabu cha Isaya 43:7: “Kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya utukufu wangu; mimi nimemwumba, naam, mimi nimemfanya.”

Atzilut maana yake ni ukaribu (‘jina langu na utukufu wangu’). Beriah maana yake ni uumbaji (‘niliyemwumba’). Yetzirah maana yake ni ufanyaji wa jambo (‘nimemfanya’). Asiyah maana yake ni tendo la kufanya jambo.

Ulimwengu wa roho hujulikana pia kama ABiYA, ambacho ni kifupi cha majina ya sayari zake tano.

Kwa nini tulizaliwa bila kuomba? Kwa nini wakati tunazaliwa hatukuwa na uhuru wa kuchagua tuzaliwe wapi au tuzaliwe kwa wazazi gani? Watu wengi wangependa kuzaliwa katika nchi nzuri au kwa wazazi wenye pesa. Lakini hivyo sivyo ilivyokuwa na haitaweza kuwa hivyo. Kwani asili yetu ni sehemu ya usawa wa ulimwengu huu na usawa wa asili ya maisha yetu.

Sisi ni watumwa; hatuna uhuru; na kwa bahati mbaya tutaendelea kuwa hivyo hadi mwisho wa dunia, kwa sababu hatuna uwezo wa kubadili asili yetu ya kibinadamu tukiwa ulimwenguni. Tunao uwezo wa kufanya hivyo tukiwa katika ulimwengu wa roho.

Hivyo, kuwa huru, kuwa raia wa ulimwengu wa roho. Ukitaka kuwa raia wa ulimwengu wa roho, kuwa rafiki (wa kweli) wa Neno la Mungu.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...