Wednesday 1 November 2017

CS-Moscow

CS-Moscow, tawi la Kolonia Santita lililotawala huko Urusi na katika nchi za Ulaya ya Mashariki kama vile Belarusi, Moldova na Ukraini; na katika baadhi ya nchi za Ulaya ya Kusini kama vile Masedonia, Montenegro, Uturuki na Ugiriki, liliongozwa na mwanajeshi wa zamani wa “Red Army” Dmitri Olegushka. Aidha, Olegushka alikuwa mwanachama hai wa zamani wa genge hatari zaidi la kimafia duniani liitwalo Solntsevskaya Bratva.

Dmitri Olegushka alikuwa na umri wa miaka 42 mwaka 1992, wakati Operation DC ikitekelezwa duniani kote, na alipigana dhidi ya Tume ya Dunia mwanzo hadi mwisho akiwa nchini Urusi. Olegushka hakuwa na umbo kubwa. Alikuwa mfupi. Alikuwa na nywele fupi nyeusi, uso mpana usiokuwa na ndevu na kitambi kidogo kilichomkaa vizuri. Alikuwa na mke na watoto wawili; na alishirikiana na Arina Gaidar, Tesak Anatoly-Chaika, Nikolay Narochnitskaya na Nakita Sergei Kerensky, kuendesha CS-Moscow. Nakita maana yake ni mtu aliyeshindikana kutekwa, lakini alitekwa nyara.

Mke wa Olegushka aliitwa Paviella. Paviella alishirikiana na mumewe kuendesha CS-Moscow, na msururu wa biashara nyingi za kimafia; wakishirikiana na magenge ya kimafia kama vile Solntsevskaya Bratva, Yamaguchi Gumi, Camorra, ‘Ndrangheta, na Sinaloa ya Amerika ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...