Monday 30 October 2017

Kidogo Kitakuwa Kikubwa

249. Katika karne hii kidogo kitakuwa kikubwa. Ukimtuma mtoto wa kizungu akupelekee taarifa, jibu unalipata mubashara.

Simu ni kifaa kidogo lakini mambo yake ni makubwa. Kuwasiliana na mtu si lazima usafiri, ambapo utatumia muda mwingi na gharama kubwa, na unaweza kujiokoa au kumwokoa mtu kwa kutumia simu.

Kabla ya kwenda kwa mtu mpigie simu, au mtumie ujumbe, kujua kama yupo au hayupo au kama anaweza kukusaidia au hawezi, kuokoa muda na pesa na hata maisha, lakini ukiitumia vibaya itakupoteza.

Teknolojia ni maarifa; ilianzishwa na Adamu na Hawa katika Bustani ya Edeni, baada ya Adamu na Hawa kutenda dhambi. Ukiona teknolojia imekuwa maarufu sana duniani, ukiona mtu amekuwa maarufu sana duniani, nyuma yake kuna dhambi kubwa.

Ndani ya teknolojia kuna dhambi kuu saba ambazo ni kiburi, uroho, zinaa, wivu, pesa, hasira, na uvivu. Kila dhambi inatufanya tujisikie vizuri. Tuimie teknolojia vizuri na kwa makini sana kwa manufaa yetu ya sasa, manufaa ambayo ni mema, na kwa manufaa yetu ya baadaye.

Mungu ametupa maarifa, lakini tunapaswa kuyatumia maarifa hayo kwa umakinifu.

1 comment:

  1. Teknolojia ipo ili tuitumie lakini ukiitumia vibaya inaleta dhambi.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...