Wednesday 13 September 2017

Meza ya Mbambakofi

Meza ya Mbambakofi katika Chumba cha Usalama cha Tume ya Dunia CUTD – chumba maalumu cha mkutano cha Ofisi ya Rais wa Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya jijini Copenhagen – Kikao cha Dharura kilipofunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Tume ya Dunia Jørgen Vestergaard Laursen, saa 11:30 alasiri, bila kiongozi wa Asia-Australia kuwepo.

Katika upande wa ncha ya meza ya duaradufu ya mbambakofi, mkabala na milango ya pea ya kutokea ndani ya ofisi ya katibu muhtasi wa Rais, alikaa Versnick akiwa amezingirwa na Makamu wa Rais Jørgen Laursen kwa upande wa kulia na Mkurugenzi wa Usalama Christoffer Sortevik kwa upande wa kushoto.

Mbele kabisa ya Rais wa Tume ya Dunia, Boidin Versnick, nyuma ya milango ya ofisi ya katibu muhtasi, aliketi Msemaji wa Tume ya Dunia Ida Taico na maafisa wawili wa kiume kulia na kushoto kwake.

Makamishna wa kanda – isipokuwa Nanda, kiongozi wa Asia-Australia, ambaye bado alikuwa hajafika, kutokana na adha za usafiri – na viongozi wengine walikuwa wametulia katika viti vyao kuzunguka meza ya mbambakofi, Makamu wa Rais aliposimama na kufungua rasmi kikao cha dharura cha Tume ya Dunia.

1 comment:

  1. Mbambakofi ni mti unaotoa mbao nyekundu kwa ajili ya kutengenezea meza, milango, na kadhalika.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...