Kuna tofauti kati ya hekima na maarifa. Unaweza kuwa profesa ukawa mpumbavu, unaweza kuwa mwanafunzi ukawa na hekima.
Hekima ni sifa ya kuwa na maarifa na uzoefu na maamuzi mazuri, sifa ya kuwa na busara. Maarifa ni taarifa na ukweli na ujuzi aupatao mtu kupitia elimu au uzoefu, uelewa wa kivitendo au kinadharia wa kitu fulani. Profesa ni mtu aliyesoma sana. Mwanafunzi ni mtu anayejifunza elimu au kazi fulani.
Nukuu hii ni kwa ajili ya watu wote kuanzia shule ya awali mpaka ngazi ya stashahada, na wasomi wote kuanzia shahada mpaka ngazi ya uprofesa. Mpumbavu ni mtu anayefanya kitu cha kijinga akijua ni ujinga.
No comments:
Post a Comment