Friday, 8 September 2017

Kitu Kisichokuua Hukufanya Mpiganaji

Mungu hutumia majaribu makubwa katika maisha yetu kutukomaza na kutukamilisha. Kitu kisichokuua hukufanya mpiganaji.

Tunapaswa kujisikia furaha kuu tunapokumbana na majaribu mbalimbali katika maisha yetu, tukijua kwamba kujaribiwa kwa imani yetu hutufanya wavumilivu na wapiganaji katika Jina la Yesu, na tunapaswa kuruhusu uvumilivu katika maisha yetu kwa sababu Mungu hutumia uvumilivu huo kutukomaza na kutukamilisha.

Yakobo, mtumwa wa Mungu, na wa Bwana Yesu Kristo, kwa kabila kumi na mbili waliotawanyika; salamu. Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno. –Yakobo 1:1-4

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...