Monday, 11 September 2017

Dini ya Mungu

242. Dini ya Mungu ni zaidi ya kutunza Amri Kumi za Mungu.

Mafarisayo walizitunza Amri Kumi za Mungu lakini haki yetu lazima iizidi ya kwao (Mathayo 5:20). Tofauti moja kati ya Kristo na Mafarisayo ni kwamba haki ya Kristo ilikuwa ya kweli, wakati ya Mafarisayo haikuwa ya kweli.

Licha ya wote kuzitunza Amri Kumi za Mungu, Mfarisayo wa kweli alikuwa mwenye haki kwa kuepuka dhambi, lakini Kristo alikuwa mwenye haki kwa kutenda mema (pia) kwa maskini na kwa wasiojiweza.

Amri Kumi za Mungu ni sehemu tu ya Biblia (Kutoka 20:2-17 baadaye ikarudiwa katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati 5:6-21). Kama hicho tu ndicho tulichotakiwa kukijua, sehemu kubwa ya Biblia isingeandikwa.

Kwani kuna amri nyingine za Mungu zinazopatikana katika kitabu cha Kutoka 34:12-26 ambazo ni Amri Kumi za Agano Jipya kati ya Mungu, Musa na Israeli; na kuna mamia mengine ya sheria ambazo ziko nje ya Amri Kumi za Mungu, zile tulizozizoea.

Biblia ina jumla ya amri 613 za Mungu; ya kwanza ikipatikana katika kitabu cha Kutoka 20:2, na Kumbukumbu la Torati 5:6, na ya mwisho ikipatikana katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati 25:19.

Tuzitunze Amri Kumi za Mungu na tutende mema wakati wote kwa maskini na kwa wasiojiweza. Tuzizingatie na kuzitekeleza kwa dhati, Amri za Mungu, kama tunataka kuuona ufalme wa mbinguni.

2 comments:

  1. Mathayo 5:6: “Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.”

    ReplyDelete
  2. Ukishabatizwa, kuwa na njaa na kiu ya haki inayoletwa kwako na Roho Mtakatifu.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...