Sunday, 27 August 2017

Kushukuru Kuna Nguvu Kuliko Kuomba

Ijapokuwa maombi ya sifa yana nguvu kuliko maombi ya kushukuru, kushukuru kuna nguvu kuliko kuomba.

Maombi ya sifa huunganisha watu wa Mungu na hutayarisha njia kwa ajili ya uwezo wa Mungu katika maisha yetu. Thamani ya maombi ya sifa wakati wa matatizo ni kuimarisha imani yetu, na kuwa karibu na Mungu wetu. Mungu anataka tumpe sifa na kumshukuru kwa kila jambo, kama Mtume Paulo anavyosema katika waraka wa kwanza wa Wathesalonike 5:16-18. Kumshukuru Mungu wakati wa matatizo ni amri, si ombi.

Binti yako mwenye umri wa miaka kumi na nne kwa mfano, anaomba umnunulie gari kama ulivyofanya kwa kaka yake mwenye umri wa miaka kumi na nane. Mara ya kwanza unamwambia utamnunulia atakapofikisha umri wa miaka kumi na nane kama ulivyofanya kwa kaka yake. Lakini baada ya wiki moja binti yako anakuomba tena kitu kilekile, yaani gari. Utajisikiaje? Utakereka, sivyo? Jinsi utakavyokereka binti yako kukuomba kitu ambacho tayari ameshakuomba, ndivyo Mungu anavyokereka sisi kumwomba vitu ambavyo tayari tumeshamwomba.

Ukiomba kitu kwa mara ya kwanza Mungu amekusikia, na tayari ameshaandaa malaika wa kukuletea jibu. Unachotakiwa kufanya, baada ya kuomba, shukuru mpaka jibu lako litakapofika. Mungu huthamini zaidi maombi ya kushukuru kuliko maombi ya kuomba. Binti yako anachotakiwa kufanya baada ya kukuomba gari ni kukushukuru mpaka gari yake itakapofika, si kukuomba mpaka gari yake itakapofika.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...