Monday, 28 August 2017

Fika Katika Nchi Yako ya Ahadi

240. Kila mtu ana kipaji angalau kimoja alichopewa na Mwenyezi Mungu. Kipaji hicho lazima kitumike, ama kwa mazuri au mabaya; kwa mazuri kama Mungu anavyotaka, kwa mabaya kama Shetani anavyotaka. Tafuta kipaji chako; kupitia kipaji hicho, fika katika nchi yako ya ahadi.

Nchi yako ya ahadi ni mustakabali wa baadaye wa maisha yako uliyomo ndani ya Mpango Mkuu wa Mungu juu ya maisha yako. Kwa maneno mengine ni kadari (au ‘destiny’) ya maisha yako, iliyoumbwa pamoja na wewe, kabla Shetani hajaingilia kati na kuvuruga mpango wa Mungu na kujiwekea wa kwake.

Watu wengine hutumia vipaji vyao nusunusu, wengine hawavitumii kabisa. Kutumia kipaji chako nusunusu, au kutokukitumia kabisa, ni makosa makubwa sana ambayo mwanadamu anaweza kufanya. Mungu alikupa kipaji ili ukitumie kwa faida yako na kwa faida ya wengine. Kwa nini hukitumii?

Tatizo la kipaji ni moja. Lazima kitumike. Usipokitumia kwa mema, Shetani atakufanya ukitumie kwa mabaya bila hata kujua. Hivyo, hutaishi sawasawa na mapenzi ya Mungu, utaishi sawasawa na mapenzi ya Shetani.

Usipokitumia kipaji chako ipasavyo wapo watu watakaoathirika kwa sababu ya uzembe wako.

Tafuta kipaji chako. Kuwa na kiu au njaa ya kufikia mafanikio, kupitia kipaji hicho.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...