Saturday 29 July 2017

Dunia ni Uwanja wa Vita


Dunia ni uwanja wa vita wa vita ya dhambi ya vita ya maisha! Kuishi maisha ya kufikirika ni kushinda vita ya maisha ya vita ya dhambi. Vita ya dhambi ya vita ya maisha si vita ya kufikirika! Bila Yesu katika maisha yetu hakuna atakayeishinda.

Kuna vita za aina mbili zinazopiganwa hapa duniani: vita ya maisha na vita ya dhambi. Unaweza kushinda vita ya maisha (maisha ya raha) lakini ukashindwa vita ya dhambi (maisha ya laana). Kushinda vita ya dhambi ni lazima umkaribishe Mwana wa Mungu Mfalme wa Amani Yesu Kristo wa Nazareti Aliye Hai, kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako.

Vita ya dhambi hupiganwa katika uwanja wa akili na katika uwanja wa mwili kati ya Shetani na Mungu. Hutumia silaha kuu ya uongo na silaha kuu ya ukweli. Mungu anataka tuujue ukweli, Shetani anataka tuujue uongo. Kushinda vita ya dhambi huna budi kuvaa silaha za Mungu na kulitumia neno la lake, kama Yesu alivyolitumia kumshinda Shetani wakati akijaribiwa katika Mlima wa Majaribu wa Jangwa la Yuda.

Ni rahisi kushinda vita ya maisha na kuishi mbinguni duniani, ni vigumu kushinda vita ya dhambi na kuishi mbinguni paradiso.

Ukitaka kushinda vita ya dhambi ya vita ya maisha soma Waefeso 6:10-13: “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.”

1 comment:

  1. Baada ya Adam na Hawa kutenda dhambi katika bustani ya Edeni, kila mtu anayezaliwa anazaliwa katika dhambi. Kwa hiyo dhambi hutokana na maisha, na maisha hutokana na dhambi.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...