236. Mungu anataka tuwe matajiri wa mwili, kwani yeye ni tajiri wa mwili na alituumba kwa mfano wake, lakini maskini wa roho.
Kuwa maskini katika roho ni jukwaa ambapo tabia nyingine zote njema zinazompendeza Mungu, na kumfanya ajibu maombi yetu kwa baraka za kiroho na wakati mwingine za kimwili, hujengeka.
Kama maskini katika mwili anavyotamani kuwa tajiri katika jamii, ndivyo maskini katika roho anavyotamani kuwa tajiri katika ufalme wa Mungu. Kwa hiyo Mungu anataka tuwe maskini katika roho, ili tutamani kuwa matajiri wa milele katika ufalme wake.
Kuwa maskini katika roho hutuwezesha kujitathmini wenyewe kwa uaminifu dhidi ya Mungu. Yeye ni mfano wa kila tabia njema, mwenye akili, hekima na mwenye uwezo mkubwa wa kutufanya tuishi kwa amani na furaha hapa duniani kama huko mbinguni. Kwa sisi kuwa na mtazamo huu Mungu lazima atayarishe mpango mkuu wa wokovu, kwa sababu asili ya binadamu na kiburi chake imejikita katika njia ya kulinda himaya yake. Yaani, imejikita katika njia ya kulinda nafasi yake katika mawazo na maamuzi yake.
No comments:
Post a Comment