Monday, 22 May 2017

Usidanganywe na Matatizo

226. Mungu ni mkubwa kuliko jumla ya matatizo yote na vitu vyote alivyoviumba na ana uwezo wa kufanya kila kitu alichosema atafanya bila kupunguza au kuongeza chochote. Usidanganywe na matatizo. Amka, kabla kifo hakijakufika.

Licha ya matatizo yanayotokea tunapaswa kujua kwa imani kwamba Mungu asiyeonekana na mwenye nguvu bado yuko kwenye kiti chake cha enzi, akisimamia kila kitu kinachoendelea, huku akijua bayana kwamba mapenzi yake lazima yatimie, bila kujali watu wasiomwamini wenye upofu wa rohoni.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...