Saturday, 20 May 2017

BUNDUKI YA USHINDI KUTOKA SINGAPURI ILIYOSABABISHA BILIONEA PANTHERA TIGRISI ATEKWE NYARA, AMBAYO NI MUUNGANO WA SAR NA G3, AINA YA SAR-8

Bunduki ya Ushindi kutoka Singapuri iliyotumiwa na Frederik Mogens kupiga mkono wa Panthera Tigrisi uliokuwa na bastola ya SIG Sauer ambayo Tigrisi alitaka kuitumia kuchukua maisha yake mwenyewe, SAR-8, iliyosababisha mfalme wa madawa ya kulevya duniani atekwe nyara na kukabidhiwa kwa mamlaka za Marekani – kujibu tuhuma za kujihusisha na ukulima na usafirishaji wa kokeini kutoka katika mashamba ya msituni ya Kolombia, mpaka katika mishipa ya damu ya watoto wa Amerika.

El Tigre hakukubali kushindwa kirahisi. Bunduki yake ilipokwisha risasi alichomoa bastola na kuendelea kujibu mashambulizi lakini wote, yeye na Vijana wa Tume, wakawa wanakosana.

Kazi ya Vijana wa Tume ilikuwa kumkamata El Tigre na kumkabidhi kwa vyombo vya sheria. Haikuwa kumuua. Lakini Murphy alidhamiria kumuua kwa sababu ya Radia. Nahodha alishaondoa nyambizi zamani sana katika jitihada za kuokoa maisha yake na ya bosi wake. Lakini hakufika mbali. Risasi moja tu ya bunduki ya Mogens ilimpasua kifua, nahodha akaegemea usukani na kuingia bazarai kwa uzembe wake.

Murphy akiendelea kupambana vikali na Kahima Kankiriho, Yehuda na Mogens walizidi kumshambulia El Tigre mpaka akakata tamaa kabisa. El Tigre alinyanyua bastola yake na kujilenga lakini pisto ikakohoa kwa kuishiwa risasi. Vijana wa Tume kuona hivyo wakashtuka. Hawakujua kama bastola yake haikuwa na risasi; walijua alitaka kujiua. Hawakutaka ajiue. Kama ni kumuua wangemuua wakiwa naye katika himaya yao.

Yehuda aling’oa nyambizi na kuifuata nyambizi ya El Tigre kwa mwendo mkali; Mogens, kipindi hichohicho, akiwa na SAR, akaulenga kwa kutumia darubini (‘telescopic sight’) mkono wa El Tigre uliokuwa na bastola na kufyatua. El Tigre alianguka, huku akigumia, pisto yake ikaruka mpaka majini na kupotea.

SAR iliyotumika kumteka nyara mfalme wa madawa ya kulevya duniani Panthera Tigrisi katika Bahari ya Pasifiki inaitwa SAR-8. Ni muungano wa SAR na G3.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...