Kiswahili ni lugha rasmi ya nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda. Ni lugha isiyo rasmi ya nchi za Msumbiji, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Lugha ya Kiswahili ni mali ya nchi za Afrika ya Mashariki, si mali ya nchi za Afrika Mashariki peke yake. Pia, Kiswahili ni lugha rasmi ya Umoja wa Afrika; pamoja na Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, Kireno na Kihispania. Kiswahili ni lugha inayozungumzwa zaidi nchini Tanzania kuliko nchi nyingine yoyote ile, duniani.
Kiswahili ni lugha ya Kibantu na lugha kuu ya kimataifa ya biashara ya Afrika ya Mashariki ambayo; maneno yake mengi yamepokewa kutoka katika lugha za Kiarabu, Kireno, Kiingereza, Kihindi, Kijerumani na Kifaransa, kutoka kwa wakoloni waliyoitawala pwani ya Afrika ya Mashariki katika kipindi cha karne tano zilizopita.
Lugha ya Kiswahili ilitokana na lugha za Kisabaki za Afrika Mashariki; ambazo nazo zilitokana na Lugha za Kibantu za Pwani ya Kaskazini Mashariki za Tanzania na Kenya, zilizotokana na lugha zaidi ya 500 za Kibantu za Afrika ya Kusini na Kati.
Lugha za Kibantu zilitokana na lugha za Kibantoidi, ambazo ni lugha zenye asili ya Kibantu za kusini mwa eneo la Wabantu yaani kusini mwa Afrika ya Kusini na Kati, zilizotokana na jamii ya lugha za Kikongo na Kibenue – tawi kubwa kuliko yote ya familia ya lugha za Kikongo na Kinijeri katika bara la Afrika.
Familia ya lugha za Kikongo na Kibenue ilitokana na jamii ya lugha za Kiatlantiki na Kikongo; zilizotokana na familia ya lugha za Kikongo na Kinijeri, ambayo ni familia kubwa ya lugha kuliko zote duniani kwa maana ya lugha za kikabila.
Kikongo-Kinijeri – Kikongo-Kiatlantiki – Kikongo-Kibenue – Kibantu cha Kusini mwa Afrika ya Kusini na Kati – Kibantu – Kibantu cha Pwani ya Kaskazini Mashariki cha Tanzania na Kenya – Kisabaki – Kiswahili. Hii ndiyo familia ya lugha ya Kiswahili.
Familia ya lugha ya Kiswahili imekuwepo kwa karne nyingi. Tujifunze kuzipenda na kuzitetea lugha zetu kwa faida ya vizazi vijavyo.
Msingi wa lugha ya Kiswahili ni sarufi na msamiati wa Kibantu pamoja na maneno mengi ya Kiarabu, Kireno, Kiingereza, Kihindi, Kijerumani, Kifaransa, na kadhalika.
ReplyDelete