Ferrari haikuwa ya kawaida. Mbali na kinga ya risasi ya inchi nne, Ferrari ya Lisa ilikuwa na mwendo mkali na matairi makubwa kuliko Ferrari za kawaida. Ilikuwa na rangi tatu: nyeusi, pinki na njano zilizokuwa zikibadilika kulingana na hali ya hewa; na kadhalika ilikuwa na breki ya upepo kwa nyuma, katika buti ya aluminiamu, kwa ajili ya kuikandamiza chini wakati wa mwendo mkali, ili isiyumbe sana barabarani. Lisa peke yake ndiye aliyekuwa na gari ya namna hiyo Mexico City nzima.
Matairi ya gari ya Lisa yalikuwa makubwa kidogo kulinganisha na Ferrari Testarossa za kawaida. Ferrari Testarossa za mwanzo zilikuwa na matairi ya Michellin TRX, katika saizi ya 240/45x415 kwa matairi ya mbele na 280/45x415 kwa matairi ya nyuma. Ferrari Testarossa ya Lisa ilikuwa na matairi ya Michellin Pilot Sport, katika saizi ya 285/40x19 kwa matairi ya mbele na 285/40ZR19 kwa matairi ya nyuma, yaliyotengenezwa Ufaransa barani Ulaya.
285 – Upana wa tairi zima kwa nje na ndani kwa kipimo cha milimeta.
40 – Urefu wa ukuta wa tairi (‘profile’ au ‘aspect ratio’), yaani 40% ya 285mm.
Z – Kiwango cha mwendo mkali na uwezo wa kudumu kwa muda mrefu.
R – Muundo wa ndani ya tairi wa ‘Radial construction’, au ‘Radial-ply’.
19 – Kipenyo cha tairi na gurudumu (‘rim’) kwa inchi (au ‘inches’).
415 – Kipenyo cha tairi na gurudumu kwa milimeta (au ‘millimeters’).
Matairi yenye teknolojia ya Radial-ply (nyuzi za tairi zilizosukwa kwa mtiririko wa kutokea katikati ya kufikirika ya tairi na kusambaa tairi zima) husaidiana na breki ya upepo kwa nyuma (‘rear wing spoiler’) kukandamiza gari wakati wa mwendo mkali ili isiyumbe sana barabarani. Matairi ya Radial-ply ni imara (na hununulika sana) kwa zaidi ya asilimia 98 ya matairi yote. Gari ya Lisa hapo juu ni mfano tu wa gari ya Lisa.
Gari ya Lisa ilikuwa na uwezo wa kukimbia umbali kadhaa bila upepo licha ya matairi yake kuwa na kinga ya risasi ya inchi nne. Ilikuwa na kitu kinaitwa ‘Self-supporting run-flat tyre’ (au teknolojia ya ‘flat tyre’) kilichokuwa na uwezo wa kufanya matairi ya Ferrari yakimbie bila upepo kabisa mpaka umbali wa kilometa themanini, kwa mwendo wa kilometa themanini kwa saa.
Ferrari Testarossa ya Lisa ndiyo iliyotumiwa na Debbie kumwokoa Murphy huko Xochimilco, Mexico City. Debbie alikuwa na siri iliyobadilisha historia ya Kolonia Santita. Lisa alikuwa na gari iliyobadilisha historia ya Tume ya Dunia.
ReplyDelete