CERN, makao makuu ya shirika la utafiti wa nyuklia la bara la Ulaya karibu na Geneva nchini Uswisi, Kiongozi wa Kanda ya Afrika ya Kusini ya Tume ya Dunia Kamishna Profesa Justin Mafuru wa Tanzania alipokuwa akifanya kazi, katika jitihada za kujibu maswali mazito ya mwanzo wa ulimwengu wetu kwa kutengeneza mazingira ya mwanzo kabisa ya mlipuko wa ‘Big Bang’.
Kiongozi wa kanda ya Afrika ya Kusini ya Tume ya Dunia Kamishna Profesa Justin Mafuru alijitolea maisha yake kufanya vitu viwili vya msingi kwa ajili ya dunia: Kukomesha madawa haramu ya kulevya nchini Tanzania na duniani kwa jumla, kupitia Tume ya Dunia, na kutafuta kupitia maabara za CERN (‘Conseil EuropĂ©en pour la Recherche NuclĂ©aire’) chembe ndogo ya ‘Higgs boson’ (‘bosoni’) inayosemekana kuhusika na uzito (‘mass’) wa chembe ndogo 16 za atomu kasoro chembe ya mwanga, iliyopotea mara tu baada ya mlipuko wa ulimwengu wa ‘Big Bang’, miaka bilioni 13.75 iliyopita, kwa faida ya uanadamu.
Mimi na wewe na vitu vyote ulimwenguni ni wazito kwa sababu ya chembe ya bosoni, ambayo haionekani, inayojulikana kama ‘The God Particle’.
Wanasayansi wa CERN wamekuwa wakiitafuta bosoni (iliyojificha ndani ya ‘Higgs field’ ya ulimwengu mzima) kwa zaidi ya miaka 50 sasa, kwa bajeti ya pauni za Uingereza bilioni 6.
Chembe ya bosoni ikipatikana itawajulisha wanasayansi jinsi ulimwengu unavyofanya kazi na jinsi ulivyoumbwa, na jibu la kitendawili cha ‘Standard Model’ (litakalotoa jibu kama kweli Mungu yupo au hayupo) litapatikana.
Ndani ya sekunde moja baada ya ulimwengu wetu kuumbwa, miaka bilioni 13.7 iliyopita, chembe zote ndogo zinazopatikana ndani ya atomu zilitengenezwa. Zote hizo zimeshapatikana isipokuwa bosoni, na bosoni ndiyo ya muhimu kuliko zote.
No comments:
Post a Comment