Wednesday, 3 May 2017

Marafiki Zako wa Mwanzo ni Wazuri Kuliko Wote


Marafiki zako wa mwanzo ambao bado ni marafiki zako mpaka sasa ni wazuri kuliko wote kutokana na sababu mbalimbali: Wamekuwepo pamoja nawe katika shida na raha; wanakujua vizuri unapokuwa na furaha, na wanakujua vizuri unapokuwa na huzuni; mmezoeana kwa miaka mingi na wanaujua hata utani wako wa ndani; wanajua nini unapendelea zaidi na nini hupendelei zaidi, na wanazijua sifa zako za ushupavu na sifa zako za udhaifu.

Hata hivyo, katika maisha yetu, tunahitaji marafiki wa aina zote mbili kurahisisha maisha. Marafiki wapya hutuongezea viungo muhimu katika maisha yetu wakati marafiki wa mwanzo ni nguzo au miamba imara ya maisha yetu, na ndiyo watu hasa watakaotusaidia katika shida na raha! Usiwapoteze au usiwaache marafiki zako wa mwanzo lakini jenga mahusiano mapya. Marafiki zako wa mwanzo ni dhahabu, wa sasa ni fedha.

1 comment:

  1. Usiwapoteze marafiki zako wa mwanzo kwa sababu ya ujinga wako, wala usiwaache marafiki zako wa mwanzo kwa sababu ya ujinga wao.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...