Pete
ya dhahabu ya Debbie Patrocinio Abrego, yenye kidani chekundu cha rubi
na mawe adimu meupe ya kikunda kutoka India, iliyokuwa na usafi wa
karati 22 na uzito wa gramu 11.57; ilikuwa chachu ya mafanikio ya lengo
la Debbie na Lisa la kumlipia kisasi mchumba wa Debbie Marciano Moreno
Herrera, aliyeuwawa kwa amri ya Panthera Tigrisi huko Tijuana nchini
Meksiko.
Lengo kuu la Debbie na Lisa katika kitabu cha Kolonia Santita
ni kumuua Kiongozi wa Kolonia Santita Panthera Tigrisi, kwa sababu
Panthera Tigrisi alimuua kinyama mchumba wa Debbie Marciano Moreno
Herrera. Bila pete ya dhahabu mwanasesere wa nyoka wa Lisa asingetambaa.
John Murphy asingepona. Lengo la Debbie na Lisa lisingefanikiwa.
No comments:
Post a Comment