Monday, 1 May 2017

Kura Yako ni Sauti Yako

223. Kura ni haki yako ya msingi kabisa kwa ajili ya maendeleo yako na ya nchi yako. Ongea na nchi yako. Yaani, chagua kiongozi atakayeweza kukuletea maendeleo. Kama hujachagua mtu, usimlalamikie yule aliyechaguliwa.

Kwa vile kura yako ni sauti yako ongea na nchi yako kwa kupiga kura sahihi bila kukosea au bila shinikizo la rushwa au dini au kabila au ushabiki, kwa ajili ya maendeleo yako na ya nchi yako.

Ukimpigia mtu kura kwa sababu za kishabiki, kikabila, kidini, kirafiki au rushwa, umeshindwa kuongea na nchi yako kama inavyopaswa, umeshindwa kuwa mzalendo wa kweli, usimlalamikie yule aliyechaguliwa.

Kama umechagua mtu akashinda au akashindwa na matokeo yakatangazwa, idadi kubwa ya watu ikakubaliana na matokeo hayo, umeongea na nchi yako na imekujibu.

Tume ya uchaguzi ikiidhinisha matokeo halafu watu wakalumbana hayo ni matatizo yenu. Nchi imeshatoa maamuzi yake.

1 comment:

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...