Monday, 29 May 2017

Mbegu ni Neno la Mungu

227. Mbegu ni neno la Mungu na kudondoka kwake kwenye ardhi si mwisho wa maisha yake. Mambo kadha wa kadha yanaweza kutokea yanayoweza kuathiri ukuaji wa mbegu husika. Nyingine zinaweza kuanguka karibu na njia ndege wakaja wakazila, nyingine zinaweza kuanguka penye miamba pasipokuwa na udongo mwingi wa kutosha, nyingine zinaweza kujifukia ndani kabisa ya ardhi na kupotelea huko kwa miaka mingi, mvua inaweza kunyesha na kuhamisha baadhi ya mbegu kwa kuzisomba na maji. Lakini kwa kuwa maisha yamo ndani ya mbegu, jambo fulani litatokea.

Katika karne iliyopita, wanaakiolojia waligundua mbegu za pamba na ngano katika baadhi ya makaburi waliyokuwa wakiyafukua kwa ajili ya utafiti wao wa kisayansi. Mbegu hizo, zilizokadiriwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 2000 hadi 4000, zilimea na kukua zilipopandwa katika udongo sahihi wenye rutuba. Roho ya maisha ilikuwa bado imo ndani ya mbegu hizo, pamoja na kwamba zilikosa mvua na jua kwa zaidi ya miaka 2000.

Huu ni uthibitisho kwamba kama mbegu itapandwa, itamea na kukua kama itapandwa katika udongo sahihi wenye rutuba. Matumizi sahihi, watu ni ardhi na mazingira yetu na kile tunachokifanya baada ya kupanda mbegu ni neno la ukweli ambalo ndani yake kuna kanuni na mafundisho ya Mungu, ndicho kinachoathiri matumizi ya mbegu.

Mbegu ni neno la Mungu. Mfano bora, msamaha, ndoto, tabasamu, uadilifu, uaminifu, uchapakazi na uvumilivu ni maneno ya Mungu. Kwa hiyo mfano bora, msamaha, ndoto, tabasamu, uadilifu, uaminifu, uchapakazi na uvumilivu ni mbegu. Watu ni ardhi. Panda mbegu ya mfano bora kwa watoto wako, msamaha kwa maadui zako, ndoto kwa malengo yako, tabasamu kwa marafiki zako, uadilifu kwa waajiri wako na kwa wafanyakazi wako pia kama unao, uaminifu kwa marafiki zako wa ukweli, uchapakazi kwa kazi zako na uvumilivu kwa wapinzani wako. Kila mbegu irutubishwe kwa imani na upendo kwa watu.

Katika mfano huu ukuaji unawakilisha utakaso, ambao ni muundo wa taswira ya Mungu ndani yetu kwa kuishi kama anavyoishi yeye kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Tunachotakiwa kufanya baada ya kupanda mbegu ni kutimiza wokovu wetu sisi wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. Kutimiza wokovu wetu sisi wenyewe ni sawa na mvua, jua, palizi, mbolea, ili mavuno yaweze kuwa ya uhakika.

Utakaso unapatikana kwa kufanya kazi. Yaani, kwa kufuata maandiko na ukweli wa Mungu.

1 comment:

  1. Ukimsamehe mtu hiyo mbegu, msamaha, itakuwa, na utatakaswa.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...