Tuesday, 18 April 2017

XM29 OICW

Bunduki iliyotumiwa na makomandoo wa Tume ya Dunia Kanali Daniel Yehuda na Sajini Radia Hosni, kubomolea majengo ya makao makuu ya Kolonia Santita duniani ya San Ángel jijini Mexico City, XM29, iliyotumia teknolojia ya OICW ya Marekani, iliyoiwezesha XM29 kufyatua makombora, yaliyokuwa na uwezo wa kulipuka hewani karibu na shabaha – hivyo kuua maadui wote, hata wale waliojificha uvunguni.

XM29 OICW ni bunduki iliyowasaidia Vijana wa Tume kubomoa jengo la utawala la Kolonia Santita katika Kiwanda cha Dongyang Pharmaceuticals jijini Mexico City, iliyowasaidia kukamata baadhi ya wakurugenzi wa Kolonia Santita kabla hawajatoroshwa na walinzi wao makomandoo.

Bunduki hii, inayotumia teknolojia ya OICW (‘Objective Individual Combat Weapon’), iliyotengenezwa na Kiwanda cha Heckler & Koch cha Ujerumani, ina uwezo wa kufyatua makombora ya HEAB (‘High Explosive Air Bursting’) yenye ukubwa wa milimeta 20.

HEAB hulipuka hewani kabla ya kugonga shabaha, kwa lengo la kusambaza vyuma vya moto katika eneo lote walipojificha maadui. Bunduki hizi hazitumiki tena. Zilitumika mara ya mwisho mwaka 2004.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...