Monday, 17 April 2017

Soma Sana

221. Soma sana. Andika sana. Ongea na watu kuhusu mambo ya muhimu unayoyafikiria. Tumia intaneti na maktaba kwa makini kwa ajili ya utafiti, kwa sababu habari nyingi za intaneti na maktaba haziaminiki. Kama una wazo kichwani mwako lizungumze kwa watu kama mazungumzo ya kawaida, ili upate maoni yao ya dhati, bila kusahau kuandika kwa siri wazo lolote jipya utakalolipata kutokana na mazungumzo hayo. Maana Mungu anaweza kuwasiliana na mtu mwingine yeyote yule akupe wazo, litakaloongeza maana zaidi katika mawazo ambayo tayari unayo.

Heshimu kila mtu. Ongea na kila mtu. Msikilize kwa makini kila unayeongea naye. Maana Mungu anaweza kumtumia mtu yeyote, hata kichaa, kukupa ufunuo wa mambo yake.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...