Falsafa hii ni ushahidi tosha kwamba Murphy hakuwa na mahusiano ya dhati na Debbie, kwani Debbie alikuwa mwembamba na Murphy anapenda wanawake waliojazia kama Sophia.
Murphy hangempenda Debbie kwa namna yoyote ile kwa dhati kwa sababu aliijua mitego ya wanawake warembo dhidi ya maadui wa Tume ya Dunia.
Mkurugenzi wa Usalama wa Tume ya Dunia alishawakanya mapema kwamba wawe makini na mitego ya wanawake na Sajini Mogens alishamwonya Murphy kuhusiana na Debbie.
Hata hivyo, bila Debbie Tume ya Dunia ingeshindwa dhidi ya Kolonia Santita.
ReplyDelete