Monday, 10 April 2017

Mlaodikia

220. Kamwe usikubali kuwa mvivu, wala usikubali kuwa mlaodikia. Usikubali starehe za dunia hii kuwa kikwazo cha maendeleo yako ya kiroho ya kadari ya maisha yako. Palilia bustani yako ya kiroho, kuondoa magugu ambayo ni raha za dunia hii.

Mbegu zilizopandwa kwenye udongo wenye rutuba ni rahisi sana kuvamiwa na magugu iwapo mwenye bustani hataipalilia bustani yake kila siku. Kila siku tunapaswa kupalilia bustani zetu za kiroho, kuondoa magugu ambayo ni raha za dunia hii.

Kama kuna jambo la muhimu unapaswa kufanya kwa ajili ya kadari ya maisha yako na kipindi hichohicho kuna kipindi kizuri cha televisheni unakisubiria, au simu ya umbea, au kinanda cha shida, palilia bustani yako ya kiroho kwa kuachana na televisheni na simu na kufanya jambo la msingi kwa ajili ya maisha yako.

Mlaodikia ni mtu anayejua kwamba bustani yake ina magugu lakini anaona uvivu kwenda kuipalilia. Kinachofanya aone uvivu kwenda kuipalilia ni raha za dunia hii. Usiwe vuguvugu. Kama umeamua kuwa moto kuwa moto. Kama umeamua kuwa baridi kuwa baridi.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...