Kibegi cha kitambaa kigumu kilichotumiwa na Vijana wa Tume kuhifadhia zana kadha wa kadha za kujiokolea na za msalaba mwekundu, Kitibegi, ambacho lengo na madhumuni yake ni kumuepusha komandoo kutoka katika makucha ya watu wabaya.
Vitibegi vya makomandoo wa Tume ya Dunia (vitibegi vya msalaba mwekundu na vitibegi vya kujiokolea) vilikuwa na vifaa maridadi vya kisasa kama vile pisto, visu, madawa ya huduma ya kwanza, kalamu za Inka, ramani za Meksiko, tochi ndogo zenye mwanga mkali za Cyba-Lite, Vioo vya TOPS, vibiriti vya Firesteel, pasi za kusafiria, pesa na vipenga vyenye viwango vya sauti vya desabo 126.
Kipenga chenye kiwango cha sauti cha desabo 126 kinaweza kupasua ngoma za masikio ya adui, na kuwajulisha Vijana wa Tume mwenzao alipo hivyo kwenda haraka na kumpa msaada.
No comments:
Post a Comment