Friday, 7 April 2017

Kuwa Mwangalifu

Neno moja kutoka mdomoni mwako linaweza kukuletea madhara makubwa. Waweza kusema kitu ukadhani umepatia kumbe umeharibu. Fikiria kwanza maana ya kitu unachosema, halafu sema.

Falsafa ya Mwangalifu inapatikana katika ukurasa wa saba wa Kolonia Santita na inamhusu moja kwa moja Kamishna wa Kanda ya Afrika ya Kusini ya Tume ya Dunia Profesa Justin Mafuru. Mafuru, akiwa ndani ya ndege ya KLM kutokea Amsterdam kuelekea Copenhagen, alikaa pembeni ya Binti wa Miami Giovanna Garcia bila kujua kama binti huyo alikuwa jambazi wa kutupwa wa Kolonia Santita.

Mafuru angesisitiza kuongea na Garcia kinyume cha wosia wa mke wake Leah, aliyemsihi awe makini na watu hasa watu asiowajua, Kolonia Santita wangepata fursa ya kumjua mapema na vizuri zaidi, hivyo kuathiri vibaya operesheni ya Tume ya Dunia ya Devil Cross.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...