Ndege anayefanana sana na mbayuwayu wa hifadhi ya taifa ya ndege ya Kalvebod Fælled au Vestamager au Amager Magharibi jijini Copenhagen, Kinegwa, alikuwa pamoja na wenzake akipiga miluzi wakati Mpelelezi wa Tume ya Dunia Daniel Yehuda akisafirishwa na majambazi wa Kolonia Santita; kutoka katika Uwanja wa Ndege wa Copenhagen mpaka katika msitu wa Kangelunden mpaka katika kisiwa cha Saltholm, kilometa nne au tano kutoka Copenhagen.
Kinegwa ni ndege mkubwa wa jamii ya mbayuwayu anayepatikana karibu na makorongo ya maji, kanda za mbuga, bahari, maziwa, mito, au sehemu yoyote iliyoko karibu na kijito. Jijini Copenhagen, Kinegwa hupatikana katika mbuga ya Kalvebod Fælled (Vestamager au Amager Magharibi – hifadhi ya taifa ya ndege, Ugandavej, Manispaa ya Tårnby). Hupatikana pia katika msitu wa Kangelunden, Msitu wa Mfalme, Vejlands Allé – karibu na Ukumbi wa Kimataifa wa Bella Center, pembezoni mwa bahari ya Baltiki.
Kinegwa – anayepatikana pia katika nchi za Afrika kama vile Kameruni, Zaire, Ethiopia, Tanzania na Afrika Kusini – hupatikana pia katika kisiwa cha Saltholm kinachotenganisha Denmaki na Swideni, Daniel Yehuda alipopelekwa na majambazi wa Kolonia Santita baada ya kutekwa nyara.
Katika riwaya ya Kolonia Santita sikutaka kuwanyima haki ya upendeleo ndege wa Tanzania kama vile Kinegwa, Kinega, Mpasuasanda na Kubo. Niliwahamisha kutoka Tanzania na kuwapeleka Denmaki.
ReplyDelete