Monday, 3 April 2017

Haki Hushindana na Sheria Unapokuwa Umeshtakiwa

219. Haki hushindana na sheria unapokuwa umeshtakiwa. Kama huna hatia lakini sheria ikasema una hatia, sheria imeishinda haki. Kama una hatia lakini sheria ikathibitisha kwamba huna hatia, sheria imeishinda haki. Kama huna hatia na sheria ikathibitisha kwamba huna hatia, sheria na haki vimelingana. Lakini kama utakata rufaa ikathibitika kwamba huna hatia, haki imeishinda sheria.

Sheria wakati mwingine inaweza kuonea mtu. Pigana hata tone la mwisho kutetea haki yako.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...