Gari la utondoti wa kiusalama wa Mtoto wa Rais wa Meksiko Debbie Patrocinio Abrego, Ford Windstar SUV, lililotumika kumlinda Debbie katika Operesheni ya Tume ya Dunia Operation Devil Cross nchini Meksiko – kutetea afya na amani ya dunia.
Gari la kifahari linalotumika katika tondoti za kiusalama za matajiri na watu wakubwa katika nchi za Amerika ya Kusini na Kaskazini, Ford Windstar SUV, lilichaguliwa na mtoto wa Rais wa Meksiko (Debbie Patrocinio Abrego) kuwa sehemu ya usalama wake popote pale atakapokuwa nchini Meksiko.
Gari hilo, la Debbie, lenye uwezo wa inchi sita za kuzuia risasi, pamoja na magari mengine manne yanayofanana au yasiyofanana na hilo, lilitumika kumlinda Debbie na mtoto wa naibu mwanasheria mkuu wa serikali (Lisa Madrazo Graciano) walipokutana na Vijana wa Tume huko Mexico City nchini Meksiko.
“Walinzi walianza kuwa na wasiwasi, lakini binti wa Ikulu akawatupia ishara akiwambia watulie. Mmoja, wa kike, hakutulia hata hivyo. Alichomoa redio, ‘walkie talkie’, na kutoka nje harakaharaka. Nje kulikuwa na magari matatu meusi – yale aliyoyaona Murphy. Mawili Windstar SUV na moja Mercedes Benz – iliyokuwa katikati.
Ndani ya magari hayo kulikuwa na walinzi watatu wa kiume, kila mmoja katika gari yake, wote wakiwa na nguo nyeusi na simu za upepo. Mlinzi wa kike, yule aliyetoka ndani, alitembea moja kwa moja mpaka katika SUV mbele ya Benz na kuongea na mmoja wa walinzi wa nje.
Hapohapo mlinzi wa nje akapiga simu ya upepo, kutumia ‘walkie talkie’, na kuongea na mtu aliyemwita kwa jina la Ramos. Ramos akaomba kupewa dakika mbili. Baada ya dakika mbili Ramos alisikika katika redio kwa sauti nzito: ‘Fuateni maelekezo ya DX. Yuko salama.’”
No comments:
Post a Comment