Usimdharau mtu aliyesaidia kukusukuma juu katika ngazi ya mafanikio yako, ikiwa utafanikiwa, kwa sababu kuna leo na kesho. Ukishuka, kama ulimdharau, hatakuamini tena. Lakini ukishuka, kama ulimheshimu, na kama bado ana uwezo wa kukupandisha juu, atakupandisha tena.
Usimdharau mtu aliyesaidia kukupa kazi ulipokuwa huna kazi, wala usimdharau mtu aliyesaidia kukulea ulipokuwa mdogo, au mtu aliyeokoa maisha yako au mtu aliyekusaidia kwa namna yoyote ile. Ukimdharau, utakaposhuka, atakusaidia kwa rehema za Mwenyezi Mungu.
No comments:
Post a Comment