Tuesday, 25 April 2017

Jesús Malverde

Jesús Malverde, jambazi sugu wa Meksiko wa karne ya kumi na tisa, mwanzilishi wa falsafa ya Yin-Yang Amerika ya Kusini na Kaskazini, anayejulikana huko Meksiko kama Jambazi Mkarimu, aliyekuwa akiiba mali kwa matajiri na kuwagawia maskini, alidumisha haki na usawa kwa watu wote.

Katika Ofisi ya Makao Makuu ya Kolonia Santita Duniani iliyoitwa Alcántara, Carlos Pulecio Alcántara, kulikuwa na Ofisi ya Siri ya Kiongozi wa Kolonia Santita Jefe de Jefes Panthera Tigrisi na makamanda wake wawili wa juu kabisa katika shirika lake la kimataifa.

Nyuma ya ‘Kiti cha Enzi’ cha Panthera Tigrisi (ukutani) kulikuwa na sanamu kubwa la chui mkubwa na mwenye nguvu kuliko wote duniani wa Siberia (Panthera Tigris) na picha kubwa ya Alphonse Gabriel ‘Al’ Capone, jambazi sugu wa Marekani wa mwanzoni mwa karne ya ishirini, kushoto kwa sanamu.

Kulia kwa sanamu kulikuwa na picha ya Jesús Malverde, jambazi sugu wa Meksiko wa mwishoni mwa karne ya kumi na tisa, shujaa wa maisha ya Eduardo Chapa de Christopher na Gortari Manuel na Panthera Tigrisi, anayeabudiwa mpaka leo na majambazi sugu na watu wengi wa kawaida katika nchi za Latino.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...