Monday, 24 April 2017

Mungu Yupo

222. Kuna watu hawaamini kama Mungu yupo, lakini maisha yao yanaamini.

Maisha ni kitu cha ajabu kuliko vyote ulimwenguni kilichowashangaza hata wanasayansi wa dunia hii. Amka na uujue ukweli.

Mungu alikupa maisha akakupa akili ili utambue jema na baya na akakupa amri zake ili uishi kwa amani na upendo. Kama Mungu hayupo mwanamume na mwanamke walitoka wapi? Wazazi wako walitoka wapi? Wazazi wao walitoka wapi? Wazazi wao walitoka wapi?

Rudi nyuma hadi kwa babu yako wa kwanza kabisa na bibi yako wa kwanza kabisa na ujiulize hata wao walitoka wapi?

Maisha tunayoishi ni ushahidi tosha kwamba Mungu yupo, na yeye ndiye aliyeanzisha maisha.

1 comment:

  1. Mungu asingekuwepo matajiri wangehonga kifo ili waishi milele.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...