Ndani ya kibweta cha risasi kuna vitu vitano vyenye uwezo wa kulipuka kama vile risasi, kasha, baruti, kitako na fataki. Risasi hutumika kama kombora, yaani kitu kinachoweza kusafiri hewani na kulipuka baada au kabla ya kugonga shabaha, wakati kasha kazi yake ni kuhifadhi vitu vyote vya kibweta kwa pamoja kusudi visisambae.
Baruti inayotoa au isiyotoa moshi ni poda yenye uwezo wa kulipuka ambayo ndani yake kuna mkaa, salfa (haluli ya chumvi) na shura (‘potassium nitrate’); ambayo husukuma kombora mbele kwa nguvu kubwa baada ya fataki kulipuka kupitia katika kitako cha kibweta. Kitako cha kibweta hutumika kama kiziduo (‘extractor’) cha risasi, kutoka katika chemba ya silaha, wakati fataki kazi yake ni kuwashia baruti.
No comments:
Post a Comment