Makao Makuu ya Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya WODEC-RANGOON, Rangoon, Bama; Kiongozi wa Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia Kamishna Meja Jenerali U Nanda wa Bama, alipopata taarifa kwa njia isiyo dhahiri ya mauaji ya Meksiko.
Meja Jenerali U Nanda, 60, Kiongozi wa Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya, alizaliwa Jumamosi ya tarehe 19/03/1932 kandokando ya mto huko Maubin nchini Bama. Yeye na familia yake ni waumini wa dini ya Ubuda. Mke wake, Daw Aung Phyu, ana miaka 57. Alizaliwa Jumapili ya tarehe 20/10/1935.
Nanda na Aung Phyu wana watoto watatu. Ko Mahn Thiri (wa kiume na wa kwanza kuzaliwa) ana miaka 37. Alizaliwa Alhamisi ya tarehe 08/12/1955. Yeye na familia yake wanakaa nchini Tailandi. Ma Nang Nyi ni mtoto wa pili wa familia ya Nanda na Aung Phyu. Alikufa kwa madawa ya kulevya Jumamosi ya tarehe 12/05/1980 akiwa na miaka 23. Alizaliwa Jumamosi ya tarehe 06/04/1957. Miaka miwili baadaye mpenzi wake wa kiume, Ko San Pe, alikufa kwa madawa ya kulevya pia Jumatano ya tarehe 21/07/1982 akiwa na miaka 25. Alizaliwa Jumanne ya tarehe 29/01/1957. Ma Thida Wai Aung ni wa mwisho kuzaliwa. Ana miaka 34. Alizaliwa Jumatano ya tarehe 23/07/1958. Anakaa Rangoon na mume wake wa miaka sita na watoto wawili, wa kike na wa kiume.
Saw Saya (Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya, kutoka katika kabila la Karen) ndiye aliyempa taarifa U Nanda za kikao cha dharura cha Tume ya Dunia. Ana miaka 54. Alizaliwa Jumanne ya tarehe 01/03/1938.
Siku za juma ni kitu cha muhimu sana katika utamaduni wa majina wa watu wa Bama.
U Nanda ni mpiganaji namba moja wa vita dhidi ya madawa ya kulevya kwa sababu ya Ma Nang Nyi na Ko San Pe, na watoto wa Bama.
No comments:
Post a Comment