Kama unataka kuijua vizuri historia ya mwanamke hasa mwanamke unayetaka kufunga naye ndoa, usifanye naye mapenzi kwa miezi sita angalau. Ukifanya naye mapenzi kwa miezi sita au zaidi, au ndani ya miezi sita, halafu akakuchanganya kimapenzi, hutakuwa na uwezo mkubwa wa kuwasikiliza watu kuhusiana na historia yake.
Watu wakikuonyesha tabia zao za ndani kabisa usisubiri wakuonyeshe tena ndiyo uwaamini. Waamini kwa mara ya kwanza. Mtu, kwa mfano, akionyesha kwa mara ya kwanza kuwa si mwaminifu mwamini. Anajijua zaidi kuliko unavyomjua. Aidha, mtu akikwambia anakupenda halafu akakupiga ni mnafiki. Maneno yake yatasema anakupenda, vitendo vyake vitasema hakupendi. Ukiwa makini na matendo ya mtu, si maneno yake, utamjua. Sikiliza maoni ya watu! Kuwa makini na matendo ya mtu.
Mwaka mmoja na nusu unatosha kumjua mwanamke kabla ya ndoa. Miezi sita itakufanya ujue kama mwanamke anaweza kuwa mchumba. Mwaka mmoja na nusu utakufanya ujue kama mwanamke anaweza kuwa mke.
No comments:
Post a Comment