Saturday, 4 March 2017

AR-15 ya Polisi wa Tume ya Dunia

Wakati AK-47 inatumiwa zaidi na majambazi wa Kolonia Santita, AR-15 inatumiwa zaidi na polisi wa Tume ya Dunia.

AR-15 ni bunduki maarufu kuliko zote katika bara la Amerika ya Kaskazini, na bunduki inayouzwa zaidi kuliko zote katika mabara ya Amerika ya Kaskazini na Kusini, ikifuatiwa na AK-47. AR-15 ina uwezo wa kubeba kwa wakati mmoja risasi 30 katika chemba yake, kupiga risasi 800 kwa dakika (kwa kutumia mkanda wa risasi), na kufyatua risasi kwa kiasi cha kuleta maafa makubwa katika umbali wa meta 548.64.

Polisi wa Tume ya Dunia hupendelea sana bunduki za AR-15 kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kufanya kazi, wepesi wake wa uzito, uwezo wake mkubwa wa kutoboa vitu vigumu, na ufasaha wake wa kulenga shabaha. Bunduki za ArmaLite Rifle-15 (AR-15) zina shabaha ya hakika zaidi (asilimia 30) kuliko bunduki za Avtomat Kalashnikova, za AK-47.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...