Friday, 10 March 2017

Kamera Haidanganyi

Kamera ina athari kubwa sana katika maisha yetu. Inaweza kuharibu taswira ya mtu mbele ya jamii, na inaweza kuharibu maisha ya mtu hali kadhalika. Wasanii wakubwa duniani hawatoki ndani bila ya kuwa nadhifu au bila ya kujipodoa. Kwa nini? Kwa sababu ya wasanii wao wa vipodozi. Wasanii wao wa vipodozi hawataki waajiri wao wawe na taswira mbaya mbele ya wateja wao ambayo ni jamii.

Kuwa na taswira mbaya mbele ya jamii kunaweza kusababisha wao wasanii wa vipodozi pamoja na wao waajiri wao wasiishi vizuri hapa duniani kama wanavyotaka. Kioo ni kitu au mtu. Kama huna uwezo wa kumiliki vipodozi, miliki kioo. Kama huna uwezo wa kumiliki kioo, miliki rafiki. Kioo (hasa kitu) hakina unafiki. Usitoke ndani bila kuridhika na taswira yako.

Robert Louis Stevenson wa Uskochi aliponukuu nahau ya “kamera haiwezi kudanganya” katika kitabu chake cha ‘South Seas’ mwaka 1896, miaka 57 baada ya sanaa ya upigaji picha kugunduliwa, hakumaanisha tuwe asilia. Hakumaanisha tusizirekebishe picha zetu baada ya kuzipiga na kuzisafisha! Alimaanisha tuwe nadhifu tuonekanapo mbele za watu au mbele ya vyombo vya habari ambapo picha itapigwa, itasafishwa, itachapishwa na itauzwa kama ilivyo bila kurekebishwa.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...