Thursday, 9 March 2017

Gari la Panthera Tigrisi Liitwalo Maserati Shamal

Gari la kifahari kutoka Italia la Kiongozi wa Kolonia Santita Panthera Tigrisi, linalokimbia kama upepo, Maserati Shamal (V8); lililotumika kumbeba Panthera Tigrisi kutoka katika Makao Makuu ya Kolonia Santita ya San Ángel, mpaka katika nyumba ya wageni ya Panthera Tigrisi ya Coyoacán, Mexico City.

Timu ya watu kumi na watano ilivyoondoka, pamoja na walinzi binafsi wa El Tigre, Gortari na Eduardo, ilitoka nje kupitia mlango wa siri mpaka yaliposimama magari sita makubwa mazuri. Eduardo na Gortari kwa pamoja walijitupa katika Lincoln Continental nyeupe na kufuatiwa na walinzi wawili wakati El Tigre akiingia katika Maserati nyeusi na walinzi watatu makomandoo. Magari yote yalikuwa na uwezo wa kuzuia risasi. Chevrolet ikiwa na walinzi wawili ilianza msafara ikifuatiwa na magari ya wakurugenzi na Chlysler ya bluu, iliyokuwa na walinzi wawili – waliokuwa na silaha kubwa walizozificha.

Maserati Tipo Birdcage (gari la mashindano la miaka ya 60, lililokuwa likihifadhiwa na Panthera Tigrisi na magari mengine zaidi ya 80, na gari gumu kuendesha kuliko yote duniani) na Maserati Shamal, ni magari ambayo Panthera Tigrisi aliyapenda zaidi kuliko magari mengine yote. Panthera Tigrisi alikamatwa katika Bahari ya Pasifiki akitoroka kuelekea Gwatemala. Maserati Shamal haikupatikana.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...