Watoto hawatakiwi kuchungwa kupita kiasi hasa katika kipindi hiki ambacho dunia imekata tamaa. Ukiwanyima watoto uhuru wa kuwa watoto leo watakuwa na uhuru wa kuwa watoto kesho. Uhuru utakaowanyima wakiwa wadogo watakuja kuutafuta baadaye wakiwa wakubwa. Wakiutafuta baadaye wakiwa wakubwa hawataeleweka vizuri katika jamii. Wape watoto uhuru wanaostahili kupata lakini si uhuru wa kila kitu.
Angalia kisa cha Marehemu Michael Jackson, aliyekuwa mwanamuziki wa Marekani. Michael Jackson hakupata uhuru wa kuwa mtoto alipokuwa mtoto, badala yake alikuwa mtoto tena alipokuwa mkubwa.
Ukiwanyima watoto nafasi ya kuwa watoto leo watakuwa watoto kesho.
Wape watoto uhuru wa mahesabu, lakini si uhuru wa shaghalabaghala.
Msichana wa miaka 8 leo anayajua maisha kwa sababu ana uhuru wa shaghalabaghala. Tuwape watoto wetu uhuru wa mahesabu.
No comments:
Post a Comment