211. Ukitaka Mungu akukumbuke jisahau!
Unaweza kuwa umeomba kuhusu jambo fulani kwa muda mrefu bila majibu, lakini siku moja ghafla ukajibiwa wakati umejisahau. Kwa nini? Kwa sababu Mungu hufanya kazi zake kwa siri. Ukiomba jambo kutoka kwa Mungu, huku ukiwa huna kinyongo na mtu yeyote na bila moyo wako kusita wakati ukiomba, tambua katika moyo wako kwamba tayari umeshajibiwa. Kisha lipotezee, hilo jambo, kila siku, usiwe unalikumbukakumbuka, hadi Mungu mwenyewe atakapokujibu. Hata Yesu atakaporudi kila mtu atakuwa amejisahau.
Shetani ni profesa wa saikolojia! Lakini, ukiwa msiri, hatakupata.
Baada ya kuomba, kila siku, huna haja tena ya kukumbuka uliloliomba. Mungu atakumbuka kwa niaba yako.
No comments:
Post a Comment