Saturday, 4 February 2017

Maabara ya Taifa ya Nguvu za Kinyukilia, Los Alamos, New Meksiko, Marekani

Mabomu ya atomiki ya ‘Fat Man’ na ‘Little Boy’ ya Marekani, yaliyoanguka Nagasaki na Hiroshima (kutokea Tinian, Marianas, Bahari ya Pasifiki) nchini Japani Agosti 1945, yalipoundwa. Na ndipo malighafi ya nyukilia ya Plutonium-239 ya Kolonia Santita, ilipoibwa na Kiongozi wa Kateli ya Madawa ya Kulevya ya Guanajuato Roberto Mosquera Portocarrero (‘El Padrino’, ‘The Godfather’), adui mkubwa wa Panthera Tigrisi.

Martin Turner Smith – mwanafizikia wa Kolonia Santita wa New Mexico nchini Marekani – ndiye aliyeiba Plutonium-239 kutoka kwa El Padrino, na hivyo kuchochea ugomvi kati ya Kateli ya Kolonia Santita na Kateli ya Guanajuato (genge la madawa ya kulevya la Tijuana na Guanajuato) wa nani atawale ukiritimba wa kokeini wa Kolombia; dhidi ya vyama haramu vya msituni vya Amerika ya Kusini. Kilo kumi za plutonium (Kolonia Santita walikuwa na kilo moja) huweza kutengeneza bomu moja la nyukilia kama la Nagasaki, na huweza kutengeneza mafuta ya kuendeshea nyambizi ya kijeshi kwa umbali wa kilometa 250000. Watu wanasema sekunde chache kabla ya kufa utayaona maisha yako mbele ya macho yako. Bomu la nyukilia likianguka (na kulipuka) mahali ulipo, hutajua uliwahi kuishi.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...