Eneo la kihistoria la vita visivyokwisha kati ya Wayahudi na Waarabu, kati ya Israeli na Palestina, Ukanda wa Gaza, Mpelelezi wa Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya Daniel Yehuda kutoka Kidon (Kitengo cha Mauti na Utekaji Nyara cha Shirika la Kijasusi la Mossad la Israeli) alipokuwa akitekeleza operesheni maalumu ya Jeshi la Israeli katika mji wa Khan Younis – faksi ya Oslo ilipofika Givat Ram, katika ofisi za Tume ya Dunia jijini Yerusalemu.
Ukanda wa Gaza ni jimbo lenye miji minne na kambi mbalimbali za wakimbizi za Umoja wa Mataifa. Lina urefu wa kati ya kilometa 41 au maili 25, na lina upana wa kati ya kilometa 6 mpaka 12 au maili 3.7 mpaka 7.5, pamoja na eneo la jumla la kilometa za mraba 365 au maili za mraba 141. Jimbo hili liliwahi kutawaliwa na Wamisri, Wakanaani, Waisraeli, Wasiria, Wababelonia, Wagiriki, Warumi, Waturuki, Waingereza, na Wapalestina, na limekuwa uwanja wa vita kwa karne nyingi kwa sababu za kidini na kihistoria. Ukanda wa Gaza uko chini ya Palestina. Uko chini ya serikali ya Hamas.
Mpelelezi wa Tume ya Dunia Daniel Yehuda kutoka Israeli alikuwa Khan Younis (ambako alikwenda kutuliza ghasia) wakati faksi ya Oslo kutoka kwa Kamishna U Nanda ilipofika ofisini kwake Givat Ram, Yerusalemu, ikimtaka aondoke haraka ilivyowezekana kwenda Rangoon na Copenhagen; kuonana na Kamishna Meja Jenerali U Nanda wa Asia-Australia na Rais wa Tume ya Dunia Boidin Versnick, kwa mfuatano huo. Alisafiri. Lakini kwa sababu ya uzembe alioufanya huko Rangoon, Yehuda alisababisha watu wengi (wenye hatia na wasiokuwa na hatia) kufa katika Machafuko ya Sheraton jijini Copenhagen.
Kama ilivyo Alaska kwa Marekani au Kaliningrad kwa Urusi ndivyo ilivyo Gaza kwa Palestina, katikati ya Mto Yordani na Bahari ya Mediterania.
Palestina ni nchi ya Waisraeli waliyopewa na Mungu wa Yakobo. Hata hivyo, hawakutimiza masharti. Mungu aliwaagiza kuua kila mtu katika nchi ya Kanaani na miji yake yote. Waisraeli, wakiongozwa na Yoshua, waliua watu wengi katika nchi ya Kanaani. Hawakuua kila mtu katika miji ya Ashdodi, Gathi na Ukanda wa Gaza kama walivyoagizwa. Mungu alimwambia Ibrahimu kuwa angempa yeye na uzao wake nchi ya Kanaani kuwa milki yao ya milele, na kuwa Yeye ndiye angekuwa Mungu wao daima. Vita ya Israeli na Palestina itamalizwa na Mungu. Itamalizwa na hekima.
Mungu alilibariki taifa la Israeli katika misingi ya kidini na si katika misingi ya kisiasa au misingi ya kihistoria; na asili ya dini ya Kikristo ni kutoka katika taifa hilo ambalo Biblia imelitaja kama Taifa Teule la Mwenyezi Mungu. Mgogoro wa Palestina na Israeli ulianzishwa na Israeli mwenyewe (Mgogoro wa Palestina na Israeli ulianzishwa na Yakobo mwenyewe). Yakobo alipokea baraka iliyokuwa si ya kwake kwa kutumia hila ya Rebeka. Baraka ya Yakobo ilikuwa ya Esau.
Hawa alimdanganya Adamu ndiyo maana tukalaaniwa. Yakobo alimdanganya Isaka ndiyo maana wakalaaniwa.
ReplyDelete