Maskini na tajiri wana mawazo tofauti. Maskini hudhani utajiri ni chanzo cha matatizo. Tajiri hudhani umaskini ni chanzo cha matatizo. Maskini hudhani ubinafsi ni kitu kibaya. Tajiri hudhani ubinafsi ni kitu kizuri.
Maskini ana mawazo ya kupata pesa bila kufanya kazi. Tajiri ana mawazo ya kupata pesa kwa kufanya kazi. Maskini hudhani tajiri ana tabia ya kuringa. Tajiri hupenda kuzungukwa na watu sahihi wenye mawazo sawa na ya kwake.
Maskini hutengeneza pesa kwa kufanya kazi asizozipenda. Tajiri hutengeneza pesa kwa kufanya kazi anazozipenda. Maskini hudhani kuwa tajiri lazima usome sana. Tajiri hudhani kuwa tajiri si lazima usome sana.
Maskini hutamani mambo mazuri ya wakati uliyopita. Tajiri hutamani mambo mazuri ya wakati unaokuja. Maskini huamini ili uwe tajiri lazima ufanye kitu fulani. Tajiri huamini ili uwe tajiri lazima uwe kitu fulani.
Maskini hupenda kuburudishwa kuliko kuelimishwa. Tajiri hupenda kuelimishwa kuliko kuburudishwa. Maskini ana woga. Tajiri hana woga.
Maskini hufundisha watoto wake jinsi ya kupambana na maisha. Tajiri hufundisha watoto wake jinsi ya kuwa matajiri. Maskini hana nidhamu ya mapato na matumizi. Tajiri ana nidhamu ya mapato na matumizi.
Maskini hufanya kazi kwa bidii kupata pesa. Tajiri hutumia pesa kupata pesa. Maskini ni mdogo kuliko matatizo yake. Tajiri ni mkubwa kuliko matatizo yake.
Maskini huamini unahitaji pesa kupata pesa. Tajiri huamini utapata pesa kwa kutumia pesa za wengine. Maskini ana wivu wa chuki. Tajiri ana wivu wa maendeleo.
Fikiri kama anavyofikiri tajiri. Ukifikiri tofauti na anavyofikiri tajiri, utakufa maskini.
Maskini: umaskini ni chanzo cha matatizo, ubinafsi ni kitu kizuri, kuwa na mawazo ya kupata pesa kwa kufanya kazi, penda kuzungukwa na watu wenye mawazo sawa na ya tajiri.
Tengeneza pesa kwa kufanya kazi unazozipenda, kuwa tajiri si lazima usome sana, tamani mambo mazuri ya wakati unaokuja, kuwa tajiri lazima uwe kitu fulani.
Penda zaidi kuelimishwa kuliko kuburudishwa, usiwe na woga, fundisha watoto wako jinsi ya kuwa matajiri, kuwa na nidhamu ya mapato na matumizi.
Tumia pesa kupata pesa, kuwa juu ya matatizo yako, amini utapata pesa kwa kutumia pesa za wengine, kuwa na wivu wa maendeleo.
Hivyo, chukia umaskini, jiangalie wewe kwanza na familia yako, fanya kazi kwa bidii na maarifa, usiwe mzururaji, tumia vipaji ulivyopewa na Mungu.
Hutafikia malengo yako kikamilifu bila msaada wa wataalamu, zifanyie kazi ndoto zako za baadaye.
Tangaza biashara yako, jinyime kwa mengi, usiogope kufanya jambo lolote lenye tija ulilolipigia hesabu, wape watoto wako kila kitu isipokuwa umaskini, mali bila daftari hupotea bila habari.
Fanya biashara, geuza matatizo yako kuwa changamoto, kopa pesa kupata pesa, kuwa na upendo kwa maskini wenzako na kwa matajiri wenzako watarajiwa.
Tajiri: bila maskini wewe ni maskini na bila tajiri maskini ni tajiri. Tajiri akiwa na maadili, maskini atakuwa tajiri.
Nukuu namba 150 na nukuu namba 151 zina uhusiano mkubwa zaidi katika Falsafa za Enock Maregesi. Kuna majuma 16, nukuu ‘zisizoonekana’ 16, kati ya nukuu namba 150 na nukuu namba 151.
Nukuu namba 150 ni kiunganishi kati ya Falsafa za Kolonia Santita na Falsafa za Enock Maregesi katika nukuu namba 151. Falsafa za Enock Maregesi zinaanza na nukuu namba 151. Nukuu namba 151 ni nukuu namba 167. Katika macho ya kawaida ni nukuu namba 151. Lakini katika macho ambayo si ya kawaida ni nukuu namba 167. Lengo lake ni kumheshimu Mungu.
Kwa hiyo ina maana Falsafa za Kolonia Santita zinaisha na nukuu namba 166 ambayo ni FIKIRI KAMA ANAVYOFIKIRI TAJIRI. UKIFIKIRI TOFAUTI NA ANAVYOFIKIRI TAJIRI, UTAKUFA MASKINI.
No comments:
Post a Comment